27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Kane: Wabaya wangu watanyamaza

harry-kane-spursLONDON, ENGLAND

BAADA ya mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane kucheza michezo sita ya Ligi Kuu nchini England msimu huu bila kupachika bao, hatimaye mwishoni mwa wiki iliyopita alifanikiwa kupata bao lake la kwanza na kusema kuwa wabaya wake watanyamaza.

Kane alifanikiwa kupachika bao moja katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Manchester City, mchezaji huyo amesema watu walikuwa na maneno mengi kutokana na mchezaji huyo kushindwa kupata bao katika michezo ya mwanzo, lakini sasa watanyamaza kwa kuwa mabao yanakuja.

Msimu uliopita mchezaji huyo alifanikiwa kushika nafasi ya pili kwa idadi kubwa ya mabao nchini England, huku akiachwa na nyota wa Manchester City, Sergio Arguero, lakini msimu huu amekuwa na wakati mgumu na kuwafanya baadhi ya mashabiki kuushangaa uwezo wake.

“Ninaamini wapo watu ambao wameanza kunyamaza baada ya kupachika bao langu la kwanza, wengi walikuwa wanaongea sana kuchelewa kwangu kupata bao, lakini naweza kusema kazi imeanza.

“Nawapa muda wa kuanza kunizungumzia baada ya kumalizika kwa michuano na ndipo waweze kutofautisha uwezo wangu wa msimu uliopita na msimu huu, lakini kwa sasa ni mapema sana kuanza kunizungumzia vibaya.

“Siyo kama sitaki kufunga mabao kama watu wanavyodhani, ninakuwa na furaha kubwa nikiwa nafunga na kuipa ushindi timu yangu, ninaamini milango ya kufunga mabao ipo wazi na nitafanya hivyo katika michezo ijayo,” alisema Kane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles