21.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Rodgers alia na wabaya wake Liverpool

brendan rodgersLIVERPOOL, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers, amesema kuwa kuna wabaya wake katika klabu hiyo ambao wanatamani aondoke, lakini anaamini ataendelea kuitumikia timu hiyo kwa muda mrefu.

Klabu hiyo imekuwa na matokeo mabaya katika michuano ya Ligi Kuu msimu huu, lakini mchezo ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Anfield mwishoni mwa wiki iliyopita, Liverpool ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Aston Villa na kuifanya klabu hiyo kushika nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi.

Hata hivyo, mashabiki wameweka wazi kuwa hawamtaki kocha huyo na ikisemekana kuwa tayari klabu hiyo imeanza kufanya mazungumzo na Carlo Ancelotti kwa ajili ya kuchukua mikoba ya kocha huyo.

Rodgers amesisitiza kuwa ana baadhi ya maadui katika klabu hiyo kutokana na matokeo mabaya yanayoendelea, lakini hana wasiwasi.

“Najua kuna maadui wengi wananizunguka kwa sasa kutokana na matokeo yaliyopo, wengine wanataka niondoke, lakini ninaamini watanyamaza muda mfupi ujao kwa kuwa ninaamini kikosi kipo sawa kwa sasa na kitafanya vizuri katika michezo ijayo.
“Lengo langu kubwa ni kupigania nafasi ya kwanza mpaka mwisho wa Ligi, kila kitu kinawezekana na ninaamini kutokana na ubora wa kikosi changu tunaweza kufanya hivyo.

 

“Kikubwa ni kunipa nafasi ili niweze kufanya kazi kama vile ambavyo watu wanataka, kila mmoja anajua nini kilitokea msimu uliopita, hivyo sasa ni wakati wa kuyafanyia kazi,” alisema Rodgers.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles