27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Arsene Wenger amjibu Jose Mourinho

wengerLONDON, ENGLAND

BAADA ya Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho kumshambulia Arsene Wenger kwamba ni kocha ambaye yupo katika wakati mgumu wa kufukuzwa na klabu yake, naye Wenger amemjibu kocha huyo kwa kusema anajivunia kuwa na jina kubwa katika chama cha soka nchini England.

Hata hivyo, Mourinho alimshambulia kocha huyo kwa kudai kuwa anapenda kuwalalamikia waamuzi wakati anapopoteza mchezo.

Wenger alionekana kumtupia lawama mwamuzi Mike Dean ambaye alichezesha mchezo wa wapinzani hao wiki moja iliyopita, huku Arsenal ikikubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Chelsea.

Lakini Wenger amesema hana wasiwasi kwa kuwa ana jina kubwa na amekuwa kwenye soka kwa miaka zaidi ya 30, hivyo ana uzoefu mkubwa.

“Najivunia kuwa nafanya kazi yangu vizuri na timu kwa ajili ya mashabiki wetu, nina uzoefu mkubwa katika soka kwa kuwa nimekuwa kwenye mchezo huu kwa miaka 30 sasa na najua umuhimu wa soka,” alisema Wenger.

Hata hivyo, kocha huyo anaamini kuwa klabu yake ina nafasi kubwa ya kuweza kuchukua ubingwa wa michuano hiyo kutokana na ushindi walioupata mwishoni mwa wiki wa mabao 5-2 dhidi ya Leicester City, huku Manchester City ambao walikuwa wanaongoza katika msimamo wa Ligi wakipokea kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Tottenham na kuwapisha Manchester United kileleni.

“Manchester City wamepoteza mchezo wao wa kwanza ambapo kwa upande wetu unatupatia nafasi ya kusogea juu, michuano ni migumu lakini tunaamini tutafanya vizuri,” aliongeza Wenger.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles