22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Kampeni za Uchaguzi Mkuu zaanza Burundi

BUJUMBURA, BURUNDI

KAMPENI za Uchaguzi Mkuu ambao umepangwa kufanyika Mei 20 zimeanza jana nchini Burundi licha ya kuwapo tishio la ugonjwa wa corona.

Kwa mujibu wa taaifa nchini humo, kampeni hizo zitamalizika Mei 17. 

Uchaguzi huo utajumuisha uchaguzi wa wabunge, madiwani na urais.

Kwa upande wa uchaguzi wa urais, wagombea saba watajaribu kuwashawishi wapigakura kwa muda wa wiki hizi tatu za kampeni. 

Jenerali Evariste Ndayishimiye, ambaye amechukua mikoba ya rais anayemaliza muda wake, Pierre Nkurunziza, atapeperusha bendera ya chama tawala cha CNDD-FDD.

Katika uchaguzi huo, Jenerali Ndayishimiye atakabiliana na Agathon Rwasa ambaye anaonekana kuwa ndiye mpinzani mkuu, akipeperusha bendera ya chama cha CNL ambacho kilisajiliwa mwaka mmoja uliopita kama chama cha siasa.

Pia Domitien Ndayizeye, rais wa mpito kati ya mwaka 2003 na mwaka 2005, naye atawania urais katika uchaguzi huo akipeperusha bendera ya muungano wa vyama – Kira Burundi. 

Kama wagombea wengine watatu, awali Ndayizeye alikataliwa kuwania katika uchaguzi huo na Tume ya Uchaguzi (CENI), lakini alishinda kesi baada ya kukata rufaa mbele ya Mahakama ya Katiba.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,502FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles