27.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Kampeni ya LGS Something Better kuwanufaisha wateja

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya uuzaji wa bidhaa zinazotumia umeme ya LG Electronics East Africa imetangaza kuzindua kampeni ya “LGs Something Better” kote nchini inayolenga kuboresha uzoefu wa ununuzi kwa wateja.

Kampeni hiyo imetangazwa leo Jumatatu Mei 23, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa LG Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim amesema kampeni hiyo inalenga kuwapa wateja punguzo la asilimia 20 kwa bidhaa zilizochaguliwa.

Mkurugenzi Mkuu wa LG Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim,

“Kwa punguzo hili la ofa, wateja wataokoa kuanzia Sh 50,000 hadi Sh 1,000,000 kwa kipindi cha wiki tano zijazo katika bidhaa zote kwenye eneo la burudani, vifaa vya nyumbani na viyoyozi vya makazi.

“Kampeni hii, inatarajia kudumu hadi Juni 12, 2022 kwa lengo la kuwapa wateja punguzo la hadi asilimjia 20 kwa bidhaa zilizochaguliwa pamoja na thamani na manufaa zaidi kwa wateja wanaonunua bidhaa kutoka kwa maduka ya chapa ya LG,” amesema Kim na kuongeza kuwa:

“Kupitia ubunifu na bidhaa zetu za hivi punde, lengo letu ni kuwasaidia wateja wetu kuishi maisha bora na rahisi zaidi. Huu ukiwa ni mwezi wa Eid al-Fitr, tunatoa nafasi kubwa kwa kila mtu kuchagua maisha haya bora sio tu ya leo bali ya kesho pia.

“Hii pia ni fursa kwa Watanzania kubadilisha na kuboresha burudani zao za nyumbani au vifaa ambavyo wamekuwa navyo kwa muda mrefu hadi kufikia teknolojia mpya, ya kisasa na vifaa vya ufanisi zaidi,” amesema Kim.

Ameongeza kuwa ofa hiyo siyo tu kwa maduka ya LG bali pia katika maduka makubwa ya Shoppers na Game Super Market.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles