26.1 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

CCM Sengerema yaahidi kutenda haki kwa wanachama

Na Anna Ruhasha, Sengerema

Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Sengerema mkoani Mwanza umewahakikishia wananchama wa chama hicho kuendelea kutenda haki na uwazi kwa kila mwanachama ambaye ataomba nafasi ya kugombea uongozi ndani ya chama.

Hayo yamebainishwa juzi na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Maki Agustine Makoye wakati akifungua mkutano maalum wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya wa kuteua wagombea ngazi za matawi.

Aidha, Makoye amesema mkutano huo maalum ni mwendelezo wa vikao vilivyopita hususan wa kuteua wagombea ndani ya chama ngazi ya matawi ambao ni Mwenyekiti, Katibu na Mwenezi.

Amesema kabla ya mkutano huo tayari ofisi yake imepitisha mapendekezo 97 ambayo hayakuathiri mapendekezo kutoka vikao ngazi ya matawi na kata.

“Naomba niwahakikishie tulichokifanya sisi tumepitia mapendekezo yote kupitia vikao vyote vya wilaya na kamati ya siasa tumepitia mapendekezo 97 ambayo mlituletea ndiyo tuliyafanyia kazi niwaombe sana viongozi wenzangu tuaminiane,”amesema Makoye.

Aidha, Makoye ametumia nafasi hiyo kupongeza kamati za siasa ngazi ya matawi na kata, halmashauri kuu ya kata na jumuiya zake tatu kwa kufanyakazi za kusimamia uchaguzi wa kupata viongozi ngazi hizo ambapo amesema ni matokeo ya kikao hicho.

Mkutano maalum wa halmashauri kuu ya CCM wilaya umeshirikisha wajumbe wa mkutano huo ambao ni kamati ya siasa ya wilaya na sekeletalieti ya wilaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles