23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

TACAIDS yapongezwa kwa kupata hati safi ya CAG

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS) imepongezwa kwa kufanya kazi nzuri na kutekeleza majukumu kwa kufuata utaratibu na kanuni zilizowekwa katika mipango yake ya utekelezaji wa shuhghuli za Tume.

Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko(aliyesimama) akitoa ufafanuzi kwa Kamisheni kuhusu umuhimu wa chama cha wafanyakazi TUGHE kwa Kamisheni,kulia kwake ni Samuel Nyungwa, Katibu TUGHE Mkoa wa Dodoma na aliyekaa kulia ni Mwenyekiti wa Kamisheni wa TACAIDS, Dk. Hedwiga Swai.

Akifungua kikao cha 49 Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk. Hedwiga Swai, amesema kuwa pamoja na mambo mengine lakini ameanza kwa kuwapongeza TACAIDS kwa kazi nzuri wanayoifanya katika utekelezaji wa majukumu ya tume.

“Nawapongeza kwa utekelezaji wa shughuli zenu kwa kufuata utaratibu na kanuni, hongereni sana, nimepata taarifa kuwa mmepata hati safi ya ukaguzi wa CAG kwani sio jambo dogo lakini naomba mwendelee kufanya hivyo msije sifiwa baada mkarudi nyuma.hongera sana Dk. Maboko na timu yako kwa ujumla,” amesema Dk. Hedwiga.

Baadhi ya watuishi wa TACAIDS wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamisheni wa TACAIDS pamoja na wafanyakazi hodari kutoka katika Idara na Vitengo vya Tume ya KUdhibiti UKIMWI Tanzania.

Dk. Hedwiga amesema amefurahishwa na jinsi ambavyo Tume imeendelea kufatilia madeni ya wafanyakazi na waliowengi wamelipwa madeni yao, jambo linaleta amani kwa watumishi kwani mtu akipata haki yake kunakuwa hakuna manung’uniko.

Naye mjumbe wa Kamisheni hiyo, Peter Maduki ameitaka tume kuhakikisha inaboresha uandishi wa taarifa kwa kuhakikisha kuwa taarifa ziwe na takwimu, Mafanikio na changamoto  zinazojitokeza ili kamisheni ione namna ya kutoa mchango wake.

Kikao cha Kamisheni kinafanyika kwa mujibu wa sheria ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania Na. 22 ya mwaka 2001 na marekebisho yake Na.6 ya mwaka 2015 kikiwa na lengo la kufatilia utekelezaji wa majukumu ya TACAIDS katika Mwitikio wa Taifa.

CPA(T) Karison Konga, (aliyeshika cheti) ambaye ni Mfanyakazi bora wa TACAIDS wa mwaka 2021 wa kwanza kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya TACAIDS, Dk. Hedwiga Swai, akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko. Kulia ni Samuel Nyungwa,Katibu TUGHE Mkoa wa Dodoma akifuatiwa na CP(T) Magreth Mrema Mwenyekiti wa Tawai la TUGHE –TACAIDS.

Baada ya kikao hicho Mwenyekiti alipata nafasi ya kukutana na baadhi ya watumishi wa Tume pamoja na wafanyakazi hodari na kuwatunuku vyeti pamoja na zawadi, ambapo mfanyakazi hodari wa jumla kutoka TACAIDS ni Mhasibu Mkuu CPA(T) Karlson Konga. 

Akiwakabidhi vyeti hivyo Dk. Hedwiga amewataka wafanyakazi wa TACAIDS kudumisha umoja na ushirikiano kwani ni kitu muhimu sana katika utekelezaji wa majukumu yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles