25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ukipeleka kuuza pamba yako ning’inia kwenye mzani-Bodi

Na Derick Milton, Simiyu

“Ili kupambana na hili tatizo, tunawataka wakulima nao watumie njia ya kujipima kwanza wenyewe kwenye hiyo mizani, mkulima ukifika na pamba yako ning’inia kwanza kwenye huo mzani uone kama uko sawa huku ukiujua uzito ulionao,” amesema Mtunga.

Bodi ya Pamba nchini imewataka wakulima wa pamba ambao watapeleka kuuza pamba kwa wanunuzi binafsi au AMCOS kuning’inia kwanza wenyewe kwenye mizani ya kupima kabla ya kupimwa pamba yao.

Kauli hiyo imetolewa Machi 24, 2022 na Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Marco Mtunga kwenye kikao cha wadau wa pamba Mkoa wa Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi, ambapo amesema kuwa iwapo wakulima watafanya hivyo hakuna mtu atakaeibiwa kupitia mizani.

Mtunga amesema kuwa eneo la mizani limekuwa na changamoto kubwa, kwani wakulima wamekuwa wakiibiwa kwa kiwango kikubwa sana na wanunuzi pamoja na viongozi wa Amcos ambapo uibiwa kati ya kilo tano hadi kumi.

“Ili kupambana na hili tatizo, tunawataka wakulima nao watumie njia ya kujipima kwanza wenyewe kwenye hiyo mizani, mkulima ukifika na pamba yako ning’inia kwanza kwenye huo mzani uone kama uko sawa huku ukiujua uzito ulionao,” amesema Mtunga na kuongeza kuwa:

“Siku hizi Serikali imejenga zahanati nyingi na vituo vya afya, tumieni hizo taasisi kujipima kwanza kujua uzito wenu, kisha peleka pamba yako Amcos au kwa mnunuzi, ukikuta mzani ning’inia kwanza wewe mwenyewe uone je? uzito ulionao ambao umepima kule zahanati au kituo cha afya ndiyo wenyewe,” amesema Mtunga.

Ameongeza kuwa licha ya serikali kupamba na tatizo hilo, kupitia wakala wa vipimo na mamlaka nyingine, bado wakulima wameendelea kuibiwa kutokana na wahusika wa wizi huo kuwa na mbinu nyingi za kucheza na mizani.

Amewataka wakulima kutumia njia ya kunin’ginia kwanza wenyewe kwenye mizani pindi watakapopeleka pamba yao kuuza, ili kutambua kama mzani unaotumika siku hiyo kama uko sahihi.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amesema kuwa katika msimu wa ununuzi wa zao hilo ambao umezinduliwa, hakuna pamba kusafirishwa usiku kama ambavyo imekuwa ikifanyika.

“Kusafirisha pamba usiku kumekuwa na matatizo mengi yakiwemo ya wizi wa pamba, kwa mkoa wa Simiyu mfumo wa ununuzi kwa mwaka huu hakuna pamba kusafirishwa usiku, mwisho kusafirisha saa 12:00 jioni,” amesema Mtunga.

Kwenye kikao hicho Mkuu wa Mkoa huo, David Kafulila amesema mkoa wa Simiyu katika msimu wa ununuzi wa mwaka huu, mfumo utakaotumika ni wa soko huru ( Milango Mingi) lengo likiwa kuongeza ushindani na kupambana na vitendo vya wizi wa pesa za wakulima ambavyo ufanywa na Amcos.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles