31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria yapitisha makadirio ya bajeti 2024/25

*Ni kwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama akizungumza wakati wa uwasilishaji wa taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Florent Kyombo akikaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo leo Machi 20, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Bungeni jijini Dodoma mara baada ya wajumbe kujadili na kuridhia Bajeti katika kikao kilichohusisha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Amesema baada ya majadiliano mazuri na maelezo ya ziada kutolewa kuhusiana na Bajeti iliyotengwa, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria imeridhia.

“Tunawatakia matumizi mema ya fedha hizi pale zitakapokubaliwa kupitishwa katika vikao vya Bunge la Bajeti na tunahitaji kuona bajeti ya fedha hizi inaakisi matarajio ya msingi ya nchi yetu,” amesema Kayombo.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Nderiananga akizungumza jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Kwa Upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Nderiananga akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ameishukuru kamati kwa ushauri na kupitia bajeti hiyo kifungu kwa kifungu na kutoa maelekezo ambayo yatasaidia Bajeti hiyo kukaa vizuri wakati kusomwa Bungeni kwenye vikao vya Bunge la Bajeti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles