31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana watakiwa kujitokeza kupata stadi za maisha Mwanza

Na Leonard Mang’oha, Mtanzania Digital

Vijana waliopata mimba za utotoni na wale walioathirika na dawa za kulevya wametakiwa kujitokeza kupata mafunzo yatakayowawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika jamii.

Wito huo ulitolewa leo Machi 19, 2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Hope for Youth Development Organization (HYDO), Anitha Samson alipozungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza.

Anitha alisema kuwa lengo la taasisi hiyo ni kuwawezesha vijana hao kukabiliana na changamoto hizo na kutambua fursa walizonazo kwenye jamii pamoja na kuwawezesha kiuchumi kupitia mafunzo ya ujasiriamali na na atadi za maisha.

Alisema lengo la taasisi hiyo ni kuwaondoa vijana kwenye matumizi ya dawa za kulevya ambayo yanachangia katika changamoto za masuala ya afya ya uzazi, maabukizi ya virusi vya Ukimwi na utoaji mimba usio salama pamoja na kuwawezesha wale waliopata mimba katika umri mdogo kujishushughulisha na shughuli mbalimbali ili na kujiepusha na mambo yatakayosababisha wapate mimba nyingine haraka.

“Tunatamani kuona wale ambapo wameingia kuona jinsi gani tunawatoa na wale ambao hawajaingia tuone jinsi gani tunawasaidia wasiingie. Kwa hiyo tunafanya kazi na taasisi mbalimbali na hospitali zinazotusaidia kutoa dawa na ushauri kwa hao vijana, pia wakati mwingine tunatoa msaada wa kisheria,” alisema Anitha na kuongeza kuwa:

“Unapoongelea afya ya uzazi ndani yake kuna ukatili wa kijinsia na unapoongelea ukatili wa kijinsia ndani yake kuna masual ya afya ya uzazi. Kwa mfano ukizungumzia ukatili wa kijinsia ni ukatili wa kijinsia unaoathiri afya ya uzazi kwa mfano mtu anaweza akakutwa na maabukizi ya virusi vya UKIMWI au majongwa ya zinaa lakini pia kuna mimba za utotoni na utoaji mimba usio salama kama njia za kujitetea kwa wale ambao wamebakwa,” aliongeza mwanaharakati huyo.

Alisisitiza kuwa watu wanaotumia dawa za kulevya hawaoni umuhimu wa afya zao hivyo wanajidunga sindano na wanafanya ngono isiyo salama hali inayosababisha kuendelea kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi na kupoteza nguvu kati ya taifa.

Mmoja wa vijana wanaonufaika na mafunzo yanayotolewa na HYDO, Neema Gervas alisema kuwa alijunga na taasisi hiyo mwaka mmoja uliopita ikiwa ni mwaka mmoja tangu alipopata ujauzito akiwa na umri wa miaka 15 hali iliyosababisha kushindwa kuendelea masomo.

Neema alisema kuwa miongoni mwa faida alizozipana ni pamoja na kupatiwa elimu ya masuala ya uzazi iliyomwezesha kujizuia kupata mimba nyingine na kuepuka magonjwa ya zinaa.

Aliwashauri vijana wengine wanaopitia changamoto mbalimbali ikiwamo waliopata mimba katika umri mdogo na wale walioathirika na matumziya dawa za kulevya kujiunga na taasisi hiyo ili kupata mafunzo yatakayowawezesha kukabiliana na changamoto hizo.

Wakipata mafunzo kama haya maisha yao yanaweza kubadilika, kwa sababu pia wametufundisha ujasiriamali. Kwa mfano mimi kwa mwaka mmoja tu tangu nimeanza kupata mafunzo haya naweza kumhudumia mwanangu, wazazi na wadogo zangu wanaosoma tofauti na mwanzo ambapo hata pesa ya kumhudumia mtoto nilikuwa nawaomba wazazi,” alisema Neema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles