20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati ya Bunge kumhoji Naibu Spika

Dk. Tulia Ackson
Dk. Tulia Ackson

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

KAMATI ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemwita Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kujieleza mbele yake kuhusu maombi yaliyowasilishwa na Mbunge wa Simanjiro, James ole Millya (Chadema)  kutaka kumwondoa madarakani.

Taarifa zilizopatikana kwa baadhi ya wabunge  Dodoma jana zilidai  Kamati hiyo tayari imemuhoji Dk. Tulia kuhusiana na suala hilo.

Habari zinasema,  Dk. Tulia alihojiwa na kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, George Mkuchika, ambayo   endapo itaridhika kwa mujibu wa kanuni, hoja hiyo itawasilishwa bungeni kwa ajili ya uamuzi wa Bunge.

Kanuni ya 138 (3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge inamtaka Spika kukalia kiti wakati wa mjadala wa hoja ya kumwondoa Naibu Spika madarakani.

Kusudio la kumwondoa Naibu Spika madarakani limepokelewa na lipo katika Ofisi ya Spika kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya kanuni.

Alipoulizwa kuhusu lini kamati hiyo itakaa na kumhoji Dk. Tulia, Mwenyekiti  wa Kamati hiyo,  Kapteni George Mkuchika alisema haruhusiwi kuzungumzia shughuli za kamati hiyo kwa vyombo habari.

“Siruhusiwi kusema nani kaitwa kwenye vyombo vya habari, Kamati yetu inafanya kazi kwa mujibu wa sheria, haturuhusiwi kusema nani kaitwa au kaandikiwa barua, subirini kazi yetu inapokuwa tayari tunaiwasilisha bungeni.

“Na hii ni kwa mujibu wa sheria siwezi kukwambia chochote hadi tutakapoimaliza,” alisema Kapteni Mkuchika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles