25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Kadi za kielekroniki kuitajirisha Simba SC

Mohamed Kassara-Dar es Salaam

UONGOZI wa klabu ya Simba umewataka wanachama, wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuhakikisha wanapata kadi mpya za kielektroniki ili kuichangia klabu yao iweze kukusanya zaidi ya Sh. Bilioni 65 kwa mwaka kupitia ada za uanachama.

Simba ilizindua mfumo mpya wa kadi kieletroni ambazo zitawawezesha wanachama kumiliki hisa za klabu yao kupitia benki, huku wakipata punguzo la bei za tiketi na jezi kila wanapoitumia kununua vifaa vyenye nembo ya Simba.

Kupitia mfumo huo mpya, klabu ya Simba inalenga kupata wanachama milioni 15 ambao wakilipa ada ya uanachama ya Sh.12, 000 kwa mwaka wataiingizia kiasi cha Sh Bilioni 65 na kuifanya Simba kuwa na bajeti kubwa ya kuiwezesha kushindana na klabu za Afrika Kaskazini.

Awamu ya pili ya uzinduzi wa kadi hizo za kielektroni unatarajia kuzinduliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, Januari 29, mwaka huu kwenye viwanja wa bunge jijini Dodoma, kisha Morogoro, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya na Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara alisema kuwa katika mkoa wa Dar es Salaam tayari baadhi ya mashabiki wameanza kujiunga kwa kuchukua kadi hizo, ambazo zitaongeza pato la klabu yao.

Alisema gharama ya kadi hiyo ni shilingi 22,000, huku shilingi 14,500 itaingia moja kwa moja kwenye mfuko wa klabu.

“Wapenzi wa klabu ya Simba Tanzania nzima mjitokeze kuchukua kadi hizi ili timu iendeshwe kisasa zaidi, hatuwezi kushindana na klabu nyingine kubwa Afrika kama tutaendelea kutegemea bajeti ndogo iliyopo sasa, hata wenzetu huko mpira ulipoendelea mashabiki wanazichangia klabu zao  ndiyo maana zinafanya vizuri.

“Tusibaki tu kulaumu wachezaji wanapokosa mabao, wewe mshabiki wa Simba usiwe shabiki oya oya, chukua kadi hii ya uanachama upate faida ya kumiliki hisa za klabu yako pendwa na kuchangia maendeleo yake.

Manara alisema baada ya Spika Ndugai kuzindua kadi hizo naye atakabidhiwa ya kwake kwakua ni mshabiki na mwanachama wa Simba pamoja na wabunge ambao wanaipenda timu hiyo ya mabingwa wa nchi.

“Januari 29, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai atazindua kadi zetu za mashabiki bungeni, lengo letu tunataka ndani ya mwaka huu tuwe tumeuza kadi laki moja kwa mashabiki,” alisema Manara.

Ili kupata kadi hiyo shabiki lazima uwe na kitambulisho cha Taifa au kile cha mpiga kura ambacho lazima uambatanishe na barua kutoka Serikali ya mtaa.

Wakati huo huo Manara alisema mchezo wao wa Kombe la Shirikisho utakaofanyika Jumamosi dhidi ya Mwadui, sasa utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa, badala ya Uhuru ambapo ulipangwa kuchezwa hapo kabla.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles