Tukuyu Stars ‘Banyambala’ tayari kuivaa JKT, yatamba kukamilika kila idara

0
934

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mabingwa wa zamani wa Soka nchini Tukuyu Star ‘Banyambala’ ya Mbeya, imetamba kuifunga Timu ya JKT Tanzania katika mchezo utakaopigwa Jumamosi Januari 25, kuwania Kombe la Shirikisho la Azam.

Tayari timu hiyo imetinga jijini Dar es Salaam ikiwa na matokeo mazuri ya mechi iliyopita baada ya kuiondosha Singida United kwenye mashindano kwa jumla ya bao 4-3 katika raundi ya tatu.

Ofisa Habari wa Tukuyu Stars, Derick Lwasye, amesema kikosi hicho kiko tayari kwa mchezo huo wa raundi ya nne na kwamba wanawaheshimu wapinzani wao lakini anakiamini zaidi kikosi chake.

“Kikosi kiko imara, tunawaheshimu wapinzani wetu lakini hatuwaogopi, hivyo wajiandae kupambana na Banyambala iliyokamilika kila idara,” amesema Lwasye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here