30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Mazingira bora ya uwekezaji ni nguzo muhimu katika sekta ya mawasiliano ya simu.

Na Mwandishi wetu.

IMMEELEZWA kuwa teknolojia ya dijitali imebadili nchi nyingi barani Afrika kwa kukua kibiashara na kuongeza tija kwenye mawasiliano, kiuchumi na kuongeza ajira nyingi mpya.

Hayo yameainishwa kwenye repoti za mitandao ya simu ambapo imeelezwa kuwa nchi yangi za Afrika maendeleo ya kidijitali yamewezekana kutokana na uwekezaji kwenye miundombinu ya mawasiliano na serikali za nchi husika kuunga mkono juhudi za sekta binafsi kisera na kimkakati.

Repoti hiyo ilsema wiki hii kampuni nguli ya teknolojia duniani ya Microsoft imetia tena msisitizo kuhusu umuhimu wa kujenga ujenzi katika teknolojia barani Afrika ili kuhakikisha bara hili linavuna faida za teknolojia siku hadi siku.

Mkurugenzi wa Microsoft kwa eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Ibrahim Youssry,amesema kampuni hiyo ni mbia wa kudumu wa bara hili katika kujenga uchumi unaotegemea maarifa, kusaidia mtaala wa elimu unaoendana na mabadiliko ya teknolojia na kujengea uwezo vijana.

Amesema Takwimu zinaonyesha kwamba toka mwaka 2017, Microsoft imesaidia vijana zaidi ya milioni barani Afrika kuongeza ujuzi na thamani katika kazi zao na hivyo kuwaweka katika mazingira bora zaidi ya kuweza kuajiriwa. Mbali na hiyo zaidi ya wajasiriamali 1,500 wanaochipukia Afrika wamewezeshwa na Microsoft kuanzisha na kuendesha biashara zao.

Amesema maendeleo hayo yanategemea ukweli kwamba ili uchumi uimarike, siku zote serikali na sekta binafsi hufanya kazi pamoja. Mfano mwezi uliopita serikali ya Nigeria na kampuni nyingine kubwa ya teknolojia duniani, IBM wametia saini makubwaliano (MoU) ya kufanya kazi pamoja kupunguza idadi ya watu ambao bado hawafaidi matunda ya kukua kwa huduma za dijitali. Makubaliano hayo yatasaidia raia wa Nigeria hasa wa vijijini.

Aliendelea kusema Tanzania karibu miongo miwili sasa kampuni binafsi zimekuwa mstari wa mbele kusaidia maendeleo ya kidijitali. Sekta ya mawasiliano ya simu imekuwa mstari wa mbele kwenye hili hasa tunapoangalia uwekezaji mkubwa ambao imefanya katika teknolojia.

Takwimu zinaonyesha sekta hii mpaka sasa imewekeza zaidi ya shilingi za Kitanzania trilioni 6.Hiki si kiwango kidogo lakini lazima kuhakikisha uwekezaji unaendelea kuongezeka ili sekta ikue zaidi na faida zake ziongezeke zaidi. Katika kuhakikisha hilo linatokea lazima kuendelea kujenga mazingira bora ya uwekezaji na biashara. Sekta hii ikikua inakuza pia sekta nyingine kama fedha, afya na ajira na nyingine, hivyo moja kwa moja inatusaidia kufikia malengo yetu kiuchumi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles