23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

KADA WA CCM AAHIDI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

Na Safina Sarwatt, Hai



Makamu Mwenyekiti wa Taifa jumuiya ya wafanyabiashara wa madini, Thomas Munisi amewaahidi wananchi wa Kata ya Machame Uroki , endapo watamchagua mgombea udiwani wa CCM Robson Kimaro, wataboresha kituo cha afya Shimbwe na kuleta vitanda vya kisasa ili wajawazito wajifungulie kwenye kituo hicho kwa Usalama.

Kada huyo wa CCM, ameyasema hayo leo wakati akifunga kampeni ya uchaguzi Mdogo wa Marudio wa udiwani Kata ya Machame Uroki, uliofanyika Katika kijiji cha Uraa Kata ya Machame Uroki.

Amesema kuwa kata hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa huduma bora za afya, ukosefu wa ajira kwa vijana, maabara katika shule ya sekondari Neema.

Kada huyo pia aliwaahidi kuwachukua vijana zaidi ya100 wasio kuwa na ajira nakuwapatia ajira.

“Mkimpigia kura mgombea wa CCM Robson Kimaro, sisi kama jumuiya ya wafanyabiashara wa madini, tutahakikisha tunashirikiana na diwani wa CCM kutatua kero zenu za ajira kwa vijana, nitachukua vijana 100 waliosoma na Wale ambao hawajasoma tuwapa kazi ili wajikwamuwe kiuchumi, “alisema.

Amesema kuwa kata hiyo ipo nyuma kimaendeleo kutokana na wananchi wake kuendelea kuwapigia kura viongozi wa upinzani wasikuona na nia njema ya kuleta maendeleo kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles