TAMASHA LA MICHEZO LINDI LAFANA

0
1167


Na HADIJA OMARY
Tamasha la michezo mkoani Lindi limezinduliwa leo na mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi kwa kushiriki mazoezi ya pamoja katika viwanja vya Ilulu manispaa ya Lindi mkoani humo.

Tamasha hilo lililoudhuliwa na viongozi mbali mbali wa mkoa na wilaya pamoja na vikindu mbalimbali vya ‘jogging’ kutoka manispaa ya Lindi na halmashauri ya wilaya ya Kilwa.
Pia wananchi wa lindi nao wamehudhuria tamasha hilo lenye lengo la kudumisha upendo na mshikamano baina ya wananchi na viongozi wa Serikali.

Kwa mujibu wa afisa michezo wa mkoa wa Lindi, Chiza Gwidegenza alisema kuwa katika tamasha hilo michezo mbalimbali imechezwa ukiwemo mchezo wa mpira wa miguu, Pete , mchezo wa bao, kukimbia na magunia, kukuna nazi kwa wanaume, kunywa soda na mkate wa boflo mbio za mita miamoja pamoja mbio za baskeli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here