25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

KABLA YA KUMUWEKA MOYONI UMEMCHUNGUZA?

MAPENZI hukamilishwa na hisia za watu wawili wanaopendana kwa dhati. Lakini lazima wawili hao wawe  na hisia sawa.

Kama upo katika uhusiano na mpenzi ambaye hakupendi, yaani wewe peke yako ndiyo unayempenda, wewe ni mtumwa wa mapenzi!

Ndiyo maana nasisitiza kuwa ili uhusiano uwe na maana lazima huyo unayeunganisha naye uhusiano awe anakupenda kwa dhati.

Kumpenda peke yako, hakuna maana. Je, umechunguza kama anakupenda kama unavyompenda au umeingia kwenye uhusiano kichwakichwa tu?

 

ANZA KWAKO KWANZA

Suala la mapenzi huhusisha moyo zaidi, moyo wako ndiyo mwamuzi wa mwisho katika hilo, hata siku moja usikubali kulazimisha moyo wako kwa mtu ambaye hujaridhia. Achana na imani kwamba ukimkataa kijana fulani basi bahati inaweza kukupita.

Suala la kuolewa halina bahati, Mungu ndiye mpangaji wa hili, unadhani hakuna mwingine ambaye anaweza kukupenda kwa mapenzi ya dhati na penzi hilo likawa kwa pande zote mbili tofauti na ilivyo sasa? Inawezekana, huna sababu ya kulazimisha penzi kwa mtu ambaye hakupendi.

Mapenzi ni nguzo katika maisha yetu, kama ukifanikiwa kumpata mpenzi ambaye atakupenda na wewe ukampenda ni wazi kuwa maisha yako yatakuwa yenye furaha na hakika utafurahia sana maisha yako na huyo mwandani wako.

Mapenzi yapo hivyo na kama ukijaribu kuyabadilisha utaumia mwenyewe. Wakati mwingine unaweza ukapendwa na mpenzi ambaye hujampenda, unadhani kuna ulazima wa wewe kulazimisha kumpenda?

Kama mtu unampenda, unapomuona tu siku ya kwanza, moyo wako hutetemeka juu yake na hutamani uambiwe kitu fulani na huyo aliyeuteka moyo wako ghafla.

Hii inamaana kuwa atakapokuambia kuwa anakupenda, huwezi kusubiri zaidi, hutakuwa na kitu cha kusubiri, ni nafasi uliyokuwa ukiisubiria kwa hamu sana, na hazima utamkaribisha.

 

USIUDANGANYE MOYO WAKO

Baadhi ya wasichana, wakitongozwa na mwanaume ambaye anaona wazi kuwa hampendi, lakini akawa na mali au uwezo mkubwa kifedha, huamua kumkubali kwa lengo la kupata vitu vya mwanaume huyo.

Hufanya hivyo akijidanganya kuwa atajifunza kupenda akiwa ndani ya uhusiano na mwanaume huyo. Baada ya wazo hili kuingia akilini, huwa hana muda wa kusubiri zaidi, anakubali na wakati mwingine huweza kuingia katika ndoa.

Huko ni kujidanganya na kuupa moyo maumivu yasiyostahili. Mwisho wa siku utajikuta ukilia mwenyewe. Kamwe huwezi kujifunza kupenda.

 

MADHARA

Yapo mengi lakini kubwa ni lile la kutokutosheka na mpenzi uliyenaye. Anaweza akakupa kila kitu lakini ukakosa penzi la dhati, ambalo ndiyo msingi wa maisha. Ukiwa na mtu anayekupenda na wewe unampenda, utajihisi furaha na amani siku zote.

Hayo ndiyo mapenzi ya kweli, siku zote hujisikia mwepesi na huru kwa mwenzako. Madhara makubwa zaidi ni pale utakapojikuta ukiingia katika uhusiano na mwanaume mwingine kwa ajili ya kusaka penzi la dhati.

Hilo ni tatizo zaidi maana matokeo ya usaliti siku zote huwa si mazuri. Matukio yanayotukia kwenye jamii yetu  yanaweza kutufunza vyema.

 

ZINGATIA ZAIDI

Kamwe usijaribu kuingia katika mkumbo huu, ni jambo gumu ambalo huweza likaharibu maisha yako kabisa. Jambo ambalo linaloweza kukusababisha ukajuta kuzaliwa.

Kuwa makini, maamuzi yahusuyo mapenzi ni lazima yafanywe kwa umakini wa hali ya juu sana. Unapofanya uamuzi juu ya mapenzi, unakuwa unapanga mustakabali wa maisha yako yajayo.

Je, unapenda kujifunza masomo haya zaidi kupitia group letu? Kama ndivyo karibu inbox, andika ujumbe wako ukitaka kujiunga na kundi hilo, nasi tutakuunganisha.

 

Jiandae kusoma kitabu changu kipya cha SIRI ZA NDOA YENYE FURAHA, kitakachoingia mitaani hivi karibuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles