MASTORI YANGU NA WAHENGA WAJAO

0
700

Na RAMADHANI MASENGA

MAKAMANDA niaje? Mambo yako supa? Kama kawa kama dawa mwanenu, mwanajeshi wa uhakika, komandoo wa kutegemewa, baharia wa nchi kavu na spai mweledi nipo nalisongesha.

Kuna wakati kutokana na haso unazopitia unajipa vyeo tu. Ama nini? Kwani unadhani Jay uprofesa alipewa pale Mlimani ama Mr II ‘Sugu’ aliwekwa kwenye karai la moto na kusavaivu ndiyo akapewa hilo jina? Haso tu wanangu.

Majita ni mafundi kinoma wa haso. Toka kitambo wanapambana na mpaka leo wanapambana. Si unaona, wakati wengine wakizama katika dimbwi la kula ngada masela wanasheki hendsi tu na mataikuni wa nchi hii!

Veri insipayaring. Dah ila kama vipi tupa kule stori za waheshimiwa aisee. Majita nimegundua mitandao ya kijamii inafanya watu wasiwe kreativu kabisa. Chukua hii.

Uko katika makundi mangapi ya WhatsApp? Tufanye matatu. Katika makundi hayo ni mara ngapi unakutana na msemo mmoja ama kituko kimoja? Yaani unaanza kukutana na msemo ama kituko fulani katika kundi ‘A’ kisha baadaye unakutana nao katika kundi ‘B’ halafu ukienda pia katika kundi ‘C’ unakutana nao.

Ni mara ngapi mambo hayo unakutana nayo? Bila shaka ni mara kibwena sio? Haya unapata picha gani? Wabongo sio wabunifu kabisa yaani. Mfano mdogo huu wa mitandao ya kijamii pia una aplai hata katika rili laifu.

Mtaani kwenu kuna mabanda mangapi ya kuuza viepe? Kuna saluni ngapi za kiume na za kike? Kisha jiulize, hao wauza viepe ama vinyozi wanapata kweli mpunga wa kutosha wa kubadili laifu zao?

Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa wanachofanya ni kugawana tu mtonyo mdogo unaopatikana. Akili kumkichwa.

Wana waliotoboa hawakuwa na mawazo kama haya. Wao walitazama ramani kisha wakaona watu wamebweteka katika mchango fulani na kusahau mwingine. Hapo hapo wakapiga mshindo wa maana.

Watu weweee. Leo wanakusanya mapesa katika maakaunti yao. Ishu ya kutokuwa kreative imezagaa hata maofisini kwetu. Kila mmoja utakuta anataka kuwa kama fulani kiutendaji ama namna yake ya kuzungumza.

Sasa wewe mwana niaje utake ufanane na mwingine wakati Saa Godi kakuumba kipekee?  Eti hata klasi ticha naye anataka mwanafunzi ajibu kama anavyotaka yeye. Kiukweli ishu isingetakiwa kuwa namna ya kujibu swali, bali kukonsetreti katika jibu kamili.

Hapo tungekuwa tunakuza hata hali ya ubunifu wa madogo wetu. Haya mambo ya kufanya tufanane kwa kila kitu ndiyo maana sasa kila kijana msomi anaota kuwa mbunge.

Mambo gani haya wanangu? Mbona kama mpunga unaweza kuuzoa hata katika Bongo Fleva ama kilimo?

Wiki iliyopita katika mitandao ya kijamii ilikuwa ni sikukuu ya wahenga. Kila kona wahenga walitrendi tu. Wakati tukifurahia habari za wahenga, umewahi kujiuliza muhenga wewe ukiwa mzee ama ukindei utaacha alama gani?

Wahenga wenzako wameacha misemo na imetrendi, wewe utaacha kitu gani ambacho kwayo utakumbukwa nacho? Au unataka ukindei ama ukizeeka tukukumbuke kwa kujua mandhari nyingi za loji?

Jipange mwanangu maana unaweza kuja kuwa mhenga wa kuwa funzo kwa wengine na siyo kuwa wa mfano. Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kuwa funzo badala ya  mfano.

Kumbuka kama na wewe ulilipa nauli shilingi hamsini wakati unasoma sekondari ni mhenga tu. Ujinga ni kama petroli katika nyasi kavu, hauchelewi kusambaa.

Ngoja nikacheki wahenga leo wana lipi jipya. Kila la kheri mhenga ujaye. Nachukua time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here