24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

K.O’s yaupamba usiku wa ‘Queen of the Ring’

Na Winfrida Mtoi, Dar es Salaam

Bondia Mtanzania, Abdallah Luanjo, amemtandika Muitaliano, Gianluca Franco kwa K.O, raundi ya nne katika pambano la utangulizi la raundi 10 la kusindikiza usiku wa ‘Queen of the Ring’ kati ya Zulfa Macho na Halima Vunjabei.

Licha ya Muitaliano huyo kuwa fiti katika raundi tatu za mwanzo, lakini kasi aliyoingia nayo Luanjo raundi ya nne kwa kumpiga makonde mfululizo ilimfanya mzungu huyo kukubali yaishe.

Mapambano mengine makali ya wanaume, George Bonabucha kutoka wa aliyempiga K.O Chiddi Mbishi raundi ya pili.

Ismail Galiatano alishinda K.O dhidi ya Nassoro Madimbo, raundi ya tano katika mpambano la raundi nane, wakati Charles Tondo alimpiga K.O Sunday Kiwale katika raundi ya tano.

Wengine ni Lolen Japhet akimpiga kwa pointi Hamisi Suleiman na Ramadhani Iddi alimtwanga Fadhili Chamile.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles