22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Zulfa Macho ndiye Malkia wa Masumbwi

Na Winfrida Mtoi, Dar es Salaam

Mtoto wa Mchezaji wa zamani wa timu ya Simba, Yusufu Macho ‘Muso’, Zulfa, ameibuka kidedea katika pambano la ngumi za kulipwa la kumsaka Malkia wa masumbwi nchini baada ya kumshinda kwa pointi Halima Vunjabei.

Zulfa alifanikiwa kutwaa ubingwa huo katika pambano la raundi 10 la ubingwa wa dunia (UBO), uzito wa ‘Super Fly’ limefanyika usiku wa kumkia leo kwenye Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.

Pambano hilo lililoandaliwa na Peaktime Media chini ya Kapteni Selemani Semunyu, ni mara ya kwanza wanawake kupigania mkanda huo.

Akizungumza baada ya kutwaa taji hilo, Zulfa, amesema kwa sasa yeye anatakiwa kutafutiwa mabondia wakubwa zaidi kwani amechoka kumpiga Halima Vunjabei.

“Nashukuru sapoti ya mashabiki zangu wote, familia pamoja na kocha wangu, lakini kwa sasa hivi mimi sio wa hadhi ya Halima tena, nimechoka kupiga,” amesema Zulfa.

Tofauti na pambano hilo, yalipigwa mengine ya utangulizi ambapo Sarafina Julius alimchapa Mwanne Haji kutoka Mbeya kwa pointi, Edna Kayage alimpiga Maimuna Hashim kwa K.O raundi ya kwanza katika pambano la raundi nne.

Wengine ni Jesca Mfinanga aliyemtwanga Lulu Kayage kwa pointi Leila Yazidu, amempiga Happy Daudi.

Fatuma Yazidu amemshinda, Dorothea Muhoza, huku Zawadi Kutaka alimchapa Martha Kimaro, wote wakishinda kwa pointi mapambano ya raundi nne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,205FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles