27.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 10, 2024

Contact us: [email protected]

JWTZ kuwasaka wanaovaa sare za majeshi

Na Ramadhan Hassan, Mtanzania Digital

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa siku saba kwa wananchi, wafanyabiashara na wasanii kuacha kutumia mavazi ya kijeshi au yanayoelekea kufanana na sare za kijeshi.

Pia, limewataka wasanii kufuata utaratibu ili kuomba kuvaa sare hizo.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Agosti 24,2023 jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi hilo, Makao Makuu Luteni Kanali, Gaudentius Ilonda wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.

Luteni Kanali Ilonda amesema wale wenye sare hizo wanatakiwa kuzipeleka kambi za jeshi, vituo vya Polisi ama kwa wenyeviti wa mitaa.

Amesema matumizi ya sare za jeshi ni kinyume cha sheria na katazo hilo ni kwa mujibu wa kifungu cha 9998 cha sheria ya ulinzi wa Taifa (NDA) sura 192 sheria namba 24 ya mwaka 1966 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Aidha, kifungu cha 178 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 (Penal Code) na kifungu cha 6 cha sheriia ya Usalama wa Taifa, vinakataza raia kuvaa sare na mavazi ya majeshi ya ulinzi au yanayofanana nayo.

“Zipo baadhi ya Taasisi zinazowashonea watumishi wake sare na aina hiyo, wapo pia wafanyabiashara wanaoingiza nchini mavazi ya aina hiyo na kuyauza kwa baadhi ya raia kupitia katika maduka au maeneo yao ta buashara, aidha wapo baadhi ya wasanii wanaovaa mavazi hayo na kuyatumia wawao kwenye majukaaa ya kazi zao bila kufuata utaratibu,” amesema Luteni Kanali Ilonda.

Amesema kumekuwa na wimbi kubwa la baadhi ya wananchi wanaokamatwa au kuonekana wakiwa wamevaa sare za jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania au mavazi yanayofanana na sare za kijeshi .

Pia, amesema mahusiano ya jeshi na wananchi ndio mhimili mkubwa ndani na nje ya nchi hivyo si hekima kulumbana kwa namna yoyote ile na baadhi ya wananchi wenye mavazi yaliyokatazwa .

“Ndio maana tunatoa siku saba kuyasalimisha bila kuchukuliwa hatua ili kuepuka usumbufu, kwa ambaye hatawasilisha atakuwa na nia ovu na dhamira mbaya,”.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanazingatia agizo hilo na wazazi wakague mabegi ya watoto wao ili kubaini kama kuna nguo ama vitu vinavyoendana na jeshi hilo ili wavisalimishe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles