25.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

AGRA yateta na Wahariri, yaipata tano Serikali

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Taasisi ya Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) ambao ni wadau wa Kilimo wamekutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini lengo likiwa ni kujenga uelewa wa pamoja kuhusu shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo.

Akizungumza leo Agosti 24, jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano huo na wahariri, Meneja Mkazi wa AGRA Tanzania, Vianey Rweyendela amesema wamekuwa hawana mikakati yao hivyo wamekuwa wakitekeleza mikakati inayowekwa na Serikali katika sekta ya kilimo

Amesema AGRA imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za kilimo na kuhakikisha sekta ya kilimo inakua na inaleta manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Kumekuwa na mafanikio makubwa yaliyopatikana kutokana na sekta hii ya kilimo ambayo imesababisha nchi kuwa na utoshelevu wa chakula,” amesema Rweyendela.

Amesema mafanikio hayo yametokana na serikali kufanya mageuzi katika sekta hiyo hali iliyosababisha kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula kwa nchi za Afrika.

“Serikali imevunja rekodi kwenye sekta ya kilimo kumekuwa na mabadiliko makubwa sana kwani sasa wakulima wanalima kwa faida,” ameongeza.

Amesema katika mkutano wa AGRF-2023, wamejipanga kuja na ripoti ya hali ya kilimo barani Afrika lakini pia kuonyesha vitu vyote vizuri vinavyofanywa na AGRA katika sekta ya kilimo.

Akizungumzia jitihada wanazozifanya kumkomboa mkulima, amesema wameboresha kwenye ununuzi wa mbegu kwa kuweka alama itakayomfanya mnunuzi kutambua ubora wa mbegu.

“Kila mbegu inayouzwa sokoni sasa hivi imethibitishwa kwa kuwekewa sehemu ya kukwangua (crach) ili kujua ubora wa mbegu wapi imezalishwa na matumizi yake,” amesema Rweyendela.

Mkutano huo umekuja ikiwa ni siku chache zimebaki kuelekea kwenye Mkutano wa Jukwaa la mifumo ya Chakula Afrika ambapo watu 3,000 wanatarajiwa kushiriki kwenye mkutano huo utakaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julias Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam Septemba 5 hadi 8 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles