28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

TARURA kuondoa vikwazo kwenye mtandao wa barabara nchini

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAKALA wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) imetaja vipaumbele kwa mwaka 2023-2024 ikiwemo kuondoa vikwazo kwenye mtandao wa barabara za Wilaya ili angalau ziweze kupitika misimu yote.

Hayo yameelezwa leo, Alhamisi Agosti 24,2023 jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Tarura, Victor Seff wakati akieleza mwelekeo wa Wakala huo kwa mwaka 2023-2024 kwa Waandishi wa Habari.

Amesema malengo ya Tarura ni barabara zilizokatika hali nzuri na hali ya wastani kubaki katika hali hiyo ili kulinda uwekezaji ambao tayari umeshafanyika.

“Matumizi ya teknolojia na malighafi za ujenzi zinazopatikana eneo la kazi (kwa mfano mawe) katika ujenzi na matengenezo ya barabara kwa lengo la kuongeza ufanisi wa gharama, kupunguza muda wa utekelezaji na kutunza mazingira,”amesema Seff.

Vilevile, kupandisha hadhi (upgrading) barabara za udongo kuwa za Changarawe/Lami kwa kuzingatia vipaumbele vya kiuchumi na kijamii, Mipango ya muda mrefu ya Kitaifa na Kimataifa, ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wa magari katika majiji, manispaa na miji.

Aidha amesema mojawapo ya kipaumbele cha TARURA ni kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi.

Amesema hadi Machi, 2023 Tarura imejenga madaraja 163 ya mawe yenye thamani ya Sh bilioni 8.7.

Amesema gharama imepungua kwa zaidi ya asilimia 50 ambapo Madaraja hayo yamejengwa katika mikoa ya Kigoma 92, Singida 24, Tabora 5, Kilimanjaro 10, Mbeya 2, Arusha 6, Mrorgoro 2, Rukwa 3, Pwani 1, Ruvuma 3 na Iringa 15.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles