23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

JPM alikuwa nguzo kwenye kuwekeza katika tafiti za zao la kahawa-TaCRI

Na Upendo Mosha,Hai

Taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa nchini (TaCRI), imesema itamkumbuka, Hayati Dk. John Magufuli katika mchango wake wa kuwekeza katika tafiti mbalimbali za zao hilo, hatua ambayo imesaidia kugundulika wa aina nyingi bora za Kahawa zenye uhakika katika soko la dunia.

Taasisi hiyo imegundua aina bora za mbegu za kahawa zenye uwezo wa kukinzana na mgonjwa mbalimbali na zenye kuhimili ukame zipatazo 23 ambapo aina ya Arabika 19 na Robusta 4.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi zake zenye makao makuu Lyamungo, wilayani Hai, mkoani,Kilimanjaro, Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa TaCRI, Dk. Deusdedit Kilambo,alisema taasisi hiyo itamkumbuka Hayati Dt. Magufuli katika harakati zake za kuinua zao la kahawa.

“Kifo cha Hayati Dkt. Magufuli ni pigo kwa taifa maana tunaelewa namna alivyokuwa na misimamo…lakini sisi kama TaCRI ambao ni watafiti wa kahawa na wasambazaji wa matokeo ya utafiti tutamkumbuka katika jitihada zake alizotusaidia na alitimiza jukumu hili kwa njia pana zaidi,”alisema.

Alisema Kahawa inalimwa katika mikoa 16 nchini na kwamba katika maeneo yote Hayati Dkt Mgufuli alihimiza wakulima kutumia matokeo ya utafiti ambayo yanaogeza tija na ubora wa Kahawa.

“Serikali imekuwa Mdau mkubwa kwa taasisi hii ambapo imekuwa ikitoa fedha na tunaamini ilikuwa ni kupitia maagizo yake… Fedha zimekuwa zikitusaidia kuendesha shughuli za utafiti na kueneza matokeo ya tafiti ambazo zimesaidia wakulima kupata tija,”alisema

Hata hivyo, Dk. Kilambo, alimpongeza Rais mpya Samia Suluhu Hassan na kumuomba kutupia jicho Katika taasisi mbalimbali za utafiti haswa za kilimo jambo ambalo litasaidia nchi kupiga hatua katika sekta ya Kokomo.

Mbali na hilo alisema jukumu kubwa la taasisi hiyo ni kutoa aina bora za kahawa zinazokidhi mahitaji ya soko ambapo kwa sasa wamefanikiwa kugundua Aina 23 bora ambapo katika nchi Afrka mashafiki wanashikilia nafasi ya Kwanza.

“Kwa Afrika mashariki tunashikilia anafasi ya kwanzaa na duniani nchi zinazofanya utafiti wa kahawa ni 60 na katika hizo sisi tunashikilia nafasi ya nane….jambo hili ni zuri na tunaimani Rais mpya Samia Suluhu ataendelea kutusaidia zaidi,”alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles