21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Mwanga abariki vyumba vya madarasa kuwa hosteli

Na Safina Sarwatt, Mwanga

Mbunge wa Jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro, Joseph Tadayo ameridhia mpango wa bodi ya shule ya Sekondari Kighare kubadilisha vyumba viwili vya madarasa kati vyumba 14 kutumika kama hosteli ya wasichana lengo nikukabilana adha ya wanafunzi kutembea zaidi ya kilomita 10.

Tadayo ametoa kauli hiyo Aprili 5,2021, wakati ziara yake katika shule sekondari Kighare iliyopo kata Kighare wilaya Mwanga nakukutana bodi pamoja walimu wa shule hiyo.

Amesema kuwa ameridhia na uamuzi wa bodi ya shule ya kubadilisha madarasa mawili kuwa hostel ya wasichana zaidi ya 40 wanaosoma shuleni hapo, wakati mchato mwingine wa kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa ukiendelea.

Amesema kuwa kukosekana kwa hosteli katika shule hiyo imekuwa changamoto kwa wanafunzi kike kutembea umbali mrefu ,na kwamba mpango huo utasaidia kuwaondolea adha hiyo pia kukabilaina na mimba shuleni na kuongeza viwango vya ufaulu wa mtihani wa taifa.

“Binafsi nimeamua kutumia muda huu wa mapumziko ya Pasaka kufanya ziara Kwenye shule za sekondari Mojawapo ni Kighare, na nimeridhia Mpango wa bodi ya shule kubadili vyumba viwili vya madarasa kuwa hostel ya wasichana 40 ,na kuanzisha mchakato wa kutafuta fedha kwa ajili ya zoezi hilo,”amesema Tadayo.

Amesema shule hiyo ina jumla ya vyumba 14 ambapo vyumba nane tu ndiyo vilikuwa vinatumika na vingine sita vilikuwa havitumiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles