24.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi toeni ushirikiano katika shughuli za kimaendeleo

Na Mwandishi Wetu, Kilimajaro

Diwani wa Kata ya Makuyuni Halmashauri ya wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Dixson Tarimo, amewataka wananchi wa Kata hiyo kutoa ushirikiano kwa kufanya shughuli za maendeleo ili kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020/2025.

Akizunguza leo na Waandishi wa habari mjini Moshi, katika kuelezea nia ya ziara yake ambayo anatarajia kuifanya kuanzia Aprili 6 hadi 18, mwaka katika kata hiyo ya ikiwa na lengo kuwashukuru wananchi wake pamoja na kusikiliza kero zao na kuwahamasisha kushiki kwenye shughuli za maendeleo.

Amesema dhamira ya ziara hiyo ni kuwashukuru wananchi kwa kukichagua CCM kwa kura nyingi zilizoifanya chama hicho kuendelea kuongoza nchi.

Amesema wananchi wanatakiwa kuhamasishana katika shughuli za maendeleo ambazo zinatekelezwa kwenye kata zilizokubali na kupitishwa na kikao Cha maendeleo ya kata.

Tarimo amesema Serikali ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, inahimiza kusogeza Huduma kwenye Jamii kwa kutekeleza ilani ya CCM walioinadi katika uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2020.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles