28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yatoa msaada wa kijamii vifaa vya Milioni 15 Hospitali za Kyela, Chunya

Na Mwandishi Wetu, Kyela

Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu imekabidhi msaada wa wa vifaa vya zaidi ya Sh milioni 15 kwa Hospitali za Wilaya za Kyela na Chunya mkoani Mbeya.

Vifaa hivyo ni mabati 204 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 6 kwa ajili ya kuezeka majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Kyela yaliyoteketea kwa moto na Vitanda 10 kwa ajili ya Kituo cha Afya Mtande Chunya vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 7.

Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Straton Chilongola akimkabidhi Afisa Tawala Wilaya ya Chunya Anacleth moja ya vitanda 10 na mashuka 30 vyenye thamani ya Sh milioni 7 kwa ajili ya Kituo cha Afya Mtande Wilayani Chunya.

Akipokea msaada wa mabati kwa ajili ya kuezeka majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Kyela Mkuu wa wilaya, Claudia Kitta, amesema kuwa Benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele kwa huduma za kijamii wilayani humo.

Kitta amesema mbali na msaada huo NMB imekwisha saidia Madawati na mabati katika shule za Msingi na Sekondari wilayani humo jambo ambalo limekuwa likiisaidia serikali katika huduma zake za kijamii.

Naye Afisa Tawala wa Wilaya ya Chunya, Anacleth Michombero, akizungumza wakati akipokea msaada wa vitanda 10 na mashuka kwa ajili ya kituo cha Mtande ameishukuru Benki ya NMB kwa kuendelea kusaidia huduma za kijamii wilayani humo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya John Mwanginde amesema kuwa Benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele kila wanapohitajika kusaidia jambo ambalo linapaswa kuigwa na taasisi zingine za kifedha.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara za Kyela na Chunya Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Straton Chilongola amesema msaada uliotolewa na Benki NMB wilayani Kyela na Chunya ni kurejesha sehemu ya faida inayopata Benki hiyo kila mwaka.

Amesema NMB imetoa mabati 204 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 6 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Kyela na Vitanda 10 na mashuka 30 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 7 kwa ajili kituo cha Afya Mtande Wilayani Chunya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles