25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Akon amepewa Ardhi Uganda

Kampla, Uganda

Waziri wa ardhi nchini Uganda Dk.Chris Barayamunsi ametangaza rasmi kutoa eneo la ukubwa wa hekari moja kwa mwanamziki mashuhuri mwenye asili ya senegal maarufu kama Akon.

Waziri Barayamusi ameyasema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari nchini humo baada ya mwanamuziki huyo kutoa ahadi ya kuwekeza fedha za kimarekani dola milioni 12 katika sekta ya mitindo nchini humo.

Pia katika mkutano huo, Akon ametoa ahadi ya kuwekeza katika sekta ya utalii, nishati na miundo mbinu chini ya kampuni yake ya Akon Lighting Afrika na kutangaza vizuri nchi ya Uganda kimataifa.

Msanii huyo amechaguwa nchi ya Uganda kuwa makao makuu ya mradi wake wa kuboresha miji barani Afrika ya Akon City Projects pia mataifa mengine yaliyopo katika mradi huo ni Senegal anakozaliwa, Ghana na Ethiopia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles