24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Miundombinu isiyo rafiki changamoto kwa wanafunzi wenye ulemavu

Na Upendo Mosh,Moshi

Ukosefu wa miundombinu isiyo rafiki kwa Wanafunzi wenye ulemavu katika shule mbalimbali nchini imetajwa kuwa ni chagamoto inayochangia kudidimiza elimu kwa watu wenye ulemavu hivyo kushindwa kufikia ndoto na malengo yao.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika lisilo kuwa la kiserikali linalojishughulisha na ulemavu kwa wanawake na watoto la Songambele, Faustina Urassa, wakati akikabidhi Masada wa vitimwendo saba kwa Wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya sekondari ya ufundi Moshi, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Alisema licha ya watoto wenye ulemavu kukabiliwa na changamoto nyingi lakini tatizo kubwa ni ukose wa miundombinu isiyo rafiki kafika shule nyingi nchini jambo ambalo limekuwa likikwamisha jitihada na harakati za kupigania haki ya kupata elimu kwa watoto walemavu.

“Tunapambana kuhakikisha watoto walemavu wanaenda shule na sasa baadhi ya wazazi wanapenda kuwapeleka shule ila changamoto tumegundua ni miundombinu sio rafiki, hatuwezi kusema waende shule bila miundombinu rafiki,”alisema Urassa

Aidha alisema miundombinu ambayo imekuwa ikikosekana katika shule ni pamoja na vyoo na viwanja vya michezo na kwamba iwapo kutakuwa na marekebisho kwa baadhi ya maeneo na kufuatwa kwa sheria ya mwaka 2016 ya walemavu sambamba na azimio la umoja wa mataifa mabadiliko yatakuwepo.

Akizungumza wakati akikabidhi Masada huyo uliotolewa na shirika hilo kwa kushirikiana na shirika mwenza la Kyaro linalojishughulisha na utengeneza vifaa vya watu wenye ulemavu, alisema wamefikia hatua ya kukabidhi vitimwendo hivyo kutokana wanafunzi hao kukosa huduma hivyo.

“tumetoa Masada huu ambao ni vitimwendo Saba na hii ni baada ya kuona badhi ya Wanafunzi wenye ulemavu wakiwa hawana viti na vingine vilikuwa vinawabana na walikuwa wakose kufanya mitihani vizuri jambo huenda wasingeweza kufanya vizuri”alisema

Katika hatua nyingine Urassa aliiomba serikali kuangalia upya kundi la walemavu kwa kutoa mikopo isiyokuwa na Masharti ya kuungana walemavu vikundi na badala yake wapatiwe mtu mmoja mmoja ili kuwainua haraka kiuchumi na kuacha maisha ya utegemezi katika jamii.

Akizungumzia shughuli zinazofanywa na shirika hilo alisema wamekuwa wakitoa elimu kwa walemavu kunikubali na kuishi na ulemavu,kuwapatia elimu ya ujasiriamali na mitaji na kutoa elimu ya afya ya uzazi na Ukimwi.

Naye Neila Karengi ambaye ni Mwanafunzi mlemavu, alisema vitimwendo hivyo vitawasaida kiafya na kukuuza ufaulu wao na kuwa huru katika kufanya shughuli zao za mara kwahiyo mara kutokana na ulemavu wao kutoonekana na kujimudu

“Tunashukuru sana shirika la Songambele name Kyaro kutusaidia vitimwendo hivi vitasaidia kurejesha furaha yetu na kuimarisha afya zetu.. Sambamba na kujiamiani zaidi vitimwendo ni sehemu ya maisha yetu,”alisema alisema Hellen Gabriel

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles