23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

JPM aagiza bil. 40/- zitolewe kulipa madeni yote ya korosho

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

RAIS  Dk. John Magufuli ameagiza Wizara ya Fedha na Mipango kutoa Sh Bilioni 40 kwa ajili ya kumalizia madeni yote ya wakulima wa korosho yaliyobaki baada ya Serikali kununua korosho za wakulima katika msimu wa mwaka 2018/19.

Rais Magufuli alitoa maagizo hayo jana, Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na viongozi wa Wizara, Mikoa, Wilaya na Taasisi za Serikali ambazo zinahusika katika uzalishaji na mauzo ya zao la Korosho mkutano ambao pia ulihudhuriwa na Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa.

Rais magufuli pia pamoja na kuagiza Wizara ya Fedha na Mipango itoe fedha hizo pia aliagiza Viongozi wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha fedha hizo zinawafikia wakulima leo na sio vinginevyo, na pia kuhakikisha wanalipwa wakulima wanaostahili kupata malipo hayo.

Aidha, rais alieleza kutoridhishwa kwake na utendaji kazi wa Wizara ya Kilimo na viongozi wa Mikoa na Wilaya ambao katika maeneo yao kumetokea wizi mkubwa wa fedha za wakulima kupitia vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) hali iliyosababisha wakulima wengi kuishi maisha duni.

“Nataka mfanye kazi, hakuna mtu wa kuwanyanyasa, nendeni mkashughulikie kero za wakulima, mna vyombo vya ulinzi na usalama nendeni mkavisimamie, kinyume na hapo nitakuona hutoshi kwenye nafasi hiyo,” alisema Rais Magufuli.

katika hatua nyingine, Rais Magufuli alisikitishwa kuona viongozi wa Wizara, Mikoa na Wilaya hawajachukua hatua madhubuti dhidi ya watu wanaowaibia wakulima hadi alipoamua kumtuma Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo, ambaye kwa muda mfupi amebaini kuwepo wizi wa shilingi Bilioni 1.23 na tayari amefanikisha kurejeshwa kwa shilingi Milioni 375 katika Mkoa wa Lindi pekee.

Aliwataka viongozi wa Wizara ya Kilimo, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kubadilika na kuhakikisha haki za wakulima zinalindwa ipasavyo kwa kurejesha fedha zilizoibwa na kuzuia mianya yote ya wizi.

“Na kuhusu minada ya korosho,nataka utaratibu uliowekwa wa kufungua mnada kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 Jioni na kisha kufungua masanduku yenye zabuni kwa uwazi mara baada ya saa 10 jioni uheshimiwe, ili kuepusha njama za upangaji wa bei,” alisema Raios Magufuli.

upande wao, Viongozi wa Mikoa na Wilaya wamemuahidi, Rais Magufuli kuwa wanakwenda kusimamia maelekezo yake na kuhakikisha haki za wakulima zinalindwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles