21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

JOTO LA UCHAGUZI LAPANDA MADAGASCAR

ANTANANARIVO, MADAGASCAR               |             


RAIS Hery Rajaonarimampianina, ametangaza kuwa atawania wadhifa huo kwa muhula wa pili mfululizo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika kati ya Novemba 7 na Desemba 19, mwaka huu kama kutakuwa na duru ya pili ya uchaguzi.

Rajaonarimampianina ambaye aliingia madarakani miaka mitano iliyopita, ameonyesha nia ya kuendelea na wadhifa huo.

“Hapa hapa nilikubaliana na nyinyi na leo nakubaliana kwa mara nyingine nanyi. Nina uhakika nitafanya zaidi kuliko niliyokufanyieni,” amesema Rais Rajaonarimampianina, mwenye umri wa miaka 59.

Katika kinyang’anyiro hicho Rais Rajaonarimampianina atapambana na wapinzani wawili na marais wa zamani, Andry Rajoelina (2009-2014) na Marc Ravalomanana (2002-2009), ambao tayari wametangaza kuwa watawania katika uchaguzi huo wa urais.

Wengine ni mawaziri wawili wa zamani, Jean Omer Beriziky na Jean Ravelonarivo, ni wagombea rasmi na Marc Ravalomanana, anatarajia kuwasilisha fomu yake siku chache zijazo. Muda wa mwisho wagombea kuwasilisha fomu zao ni Agosti 21, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles