JKT Tanzania watamba wapo tayari

0
860

Theresia Gasper-Dar es Salaam

KOCHA Mkuu wa JKT Tanzania, Abdallah Mohammed ‘Bares’, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mapambano  na kuhakikisha kinapata ushindi dhidi ya Tukuyu Stars.

Timu hizo zitashuka dimbani kuumana Januari 25 mwaka huu, katika mchezo utakaochezwa  Uwanja wa Meja Jenerali Michael  Isamuhyo, Dar es Salaam.

JKT Tanzania ilivuka hatua hiyo, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Boma.

Tukuyu kwa upande wake iliiondosha Singida United, baada ya kuinyuka mabao 4-3, Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Bares alisema wanaendelea na maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo ambao anatarajia utakuwa na ushindani mkubwa.

“Tumeingia kambini tangu juzi tunaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo huu, naamini tutafanya vizuri  kutokana na mbinu ninazowapa wachezaji wangu,” alisema. Bares alisema Tukuyu sio timu ya kubeza hivyo wataingia dimbani na tahadhari ili kuepuka kufungashiwa virago.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here