22 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Mexime aiandalia dozi nzito Might Elephant

Theresia Gasper -Dar es Salaam

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, amesema watahakikisha wanaendeleza vichapo kwa kuilaza Might Elephant, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi hii Uwanja wa Kaitaba,  Kagera.

Kagera ilifuzu hatua hiyo, baada ya kuifunga Rufiji United 4-1,  huku Might Elephant ikiiondosha Mashujaa kwa jumla ya mabao 3-1.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mexime alisema wanafanya maandalizi ya mwisho kuelekea katika mchezo huo ambao wanamini watafanya vizuri.

“Hatuwezi kuwadharau wapinzani wetu kwani lolote linaweza kutokea ila tumepanga kupata pointi tatu muhimu na kusonga mbele katika michuano hii,” alisema.

Alisema baada ya ushindi waliopata dhidi ya Yanga wanahitaji kuendeleza kutoa vichapo kwa timu watakazokutana nazo ili wafanye vizuri zaidi.

Mexime alisema wachezaji wake wapo vizuri hakuna majeruhi hadi sasa ambako kila mmoja anaonekana kufuata kile anachowafundisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles