Theresia Gasper -Dar es salaam
TIMU ya JKT Tanzania imechapwa mabao 2-0 na Zimamoto, katika mchezo wa kirafiki uliochezwa juzi.
JKT ipo Zanzibar ikijifua kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdallah Mohammed ‘Bares’, alisema anahitaji mechi zaidi za kirafiki ili kikosi chake kiweze kuimarika.
“Tumecheza mchezo mmoja dhidi ya Zimamoto lakini tumefungwa 2-0, ila ndio kwanza tumeanza kucheza mechi za kirafiki.
“Naamini tutafanya vizuri katika michezo ijayo,” alisema.
Alisema amesajili kikosi kipana ambacho anaamini kitaleta ushindani katika Ligi Kuu msimu ujao tofauti na walivyokuwa msimu uliopita.
Bares alisema kwa kipindi hiki kifupi walichoweka kambi Zanzibar, ameanza kushuhudia mabadilika ya kiuchezaji katika kikosi chake.
JKT msimu uliopita ilimaliza Ligi Kuu ikiwa nafasi ya kumi, baada yta kujikusanyia pointi 47.