23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

KMC kamili kuivaa AS Kigali kesho

Theresia Gasper -Dar es salaam

KOCHA Mkuu wa timu ya KMC , Jackson Mayanja amesema kikosi chake kipo tayari kuivaa AS Kigali, katika mchezo wao wa kwanza wa hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo huo, utapigwa kesho, Uwanja wa Nyamirambo, Kigali nchini Rwanda.

Kikosi cha KMC tayari kipo katika viunga vya jiji la Kigali, kikijifua kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuzindua kampeni zao.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mayanja alisema, wachezaji wake wana morali ya juuu ya kutaka kuhakikisha wanapata ushindi ugenini kabla ya kurejea nyumbani kumaliza kazi.

“Tupo Kigali tunaendelea na mazoezi ya mwisho japo hali ya hewa ya huku ni baridi tofauti na Dar es Salaam.

Lakini hiyo sio sababu ya kutukwamisha, lengo letu ni kuhakikisha tunapata ushindi bila kujali tunacheza ugenini,” alisema.

Aliongeza, “ Salum Aiyee ndiye anayeweza kuukosa mchezo wa kesho kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya bega.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,070FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles