26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Uchumi wa Uingereza washuka kwa mara ya kwanza tangu 2012

LONDON, UINGEREZA 

KANSELA anayeshughulikia kitengo cha ukusanyaji kodi na kudhibiti matumizi nchini Uingereza, Sajid Javid  amesema hatarajii  Uingereza kuyumba kiuchumi baada ya takwimu kuonyesha kuwa uchumi umeshuka kwa asilimia 0.2  kati ya Aprili na Juni.

Javid aliyasema hayo baada ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini humo kueleza kuwa uchumi umeshuka kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012.

Taarifa hizo zimekuja katika wakati ambao suala la Brexit likiwa limeleta sintofahamu huku baadhi ya viwanda vikifungwa kikiwamo kile cha magari.

Tayari takwimu hizo ikiwa ni pamoja na kutikisika kwa paundi ya Uingereza kumeimeibua hofu ya kushuka kwa uchumi.

Paundi ya Uingereza imetikisika kwa miezi 31 sasa dhidi ya dola kwa 1.2056, wakati dhidi ya Euro ikishuka kwa 1.0768.

Rob Kent-Smith, ambaye ni kiongozi wa GDP, alisema uzalishaji wa viwanda umeshuka na sekta ya ujenzi nayo imedhoofika.

Baadhi  wanaona kuwa kushuka huko kwa uchumi kumechangiwa na mchakato wa Brexit jambo ambalo pia limegusiwa na Sajid.

“Ni kweli kuna biashara ambazo zinaguswa na Brexit wakati ambapo maamuzi yanafanyika,” alisema Sajid.

Alisema hakuna mtu ambaye atashangazwa na takwimu hizo.

Takwimu hizo zimekuja katika wakati ambao tayari dalili za kushuka kwa uchumi zilianza kuonekana.

Kwa mfano takwimu zilizotolewa jana zilionyesha kuwa bidhaa za viwandani za Ufaransa zilishuka kuliko ilivyotarajiwa mwezi Juni.

Pamoja na hayo Javid anasema “Hiki ni kipindi kigumu katika uchumi wa dunia, huku ukuaji wa uchumi ukionekana kushuka katika mataifa mengi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles