28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Jiji la Dodoma latakiwa kuhamasisha upandaji miti

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

JIJI la Dodoma limetakiwa kuhamasisha upandaji wa miti kwa kuhakikisha kila mwenye kiwanja katika Jiji hilo anapanda miti angalau 20 kwa mwaka lengo likiwa ni kutunza mazingira.

Akizungumza leo Alhamisi Februari 10,2022 wakati wa zoezi la usafi katika soko la Mavunde lilopo Chang’ombe jijiji hapa, Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Dk. Godwin Mollel amesema anashangaa Jiji hilo kuhamasisha upakaji rangi katika mapaa ya nyumba kuliko uoteshaji wa miti.

“Yaani ni faraja mtu kuja nje kwako na kukuta kuna miti mingi, Dodoma najua mna watumishi wapo Halmashauri eti mmetupangia tujenge nyumba ya rangi gani kwenye mabati kwenye eneo la Dodoma mnasimamamia rangi ya mabati kuliko uoteshaji wa miti hilo nalo ni shida.

“Yaani wewe bati yangu nanunua mwenyewe halafu unanisimamia kuliko kupanda miti sasa jinsi ambavyo mnatumia nguvu nyingi kuwasimamia, tunawaomba nendeni mkasimamie kila mtu aoteshe hata miti 20 kwa mwaka huu si ndio jamani eeeh tutaotesha wenyewe.

“Tena kuna miti mizuri inaitwa Midodoma tukiotesha Midodoma katika shule zetu, tukubaliane kila mzazi anampa mtoto wake mti akautunze shuleni,”amesema Dk. Mollel.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mary Maganga amesema zoezi hilo lilianza Februari 7, mwaka huu ikiwa ni muendelezo wa shughuli ya wiki ya uzinduzi wa Sera hiyo na inatarajiwa kuhitimishwa Februari 12.

Kwa upande wake, Ofisa Mazingira wa Jiji hilo, Ally Mfinanga, amesema kuna umuhimu wa wananchi kutenganisha taka ikiwamo za plastiki ili kuipunguzia mzigo Halmashauri inayotumia asilimia kubwa ya fedha zake katika usafirishaji wa taka.

“Tunataka tutenganishe taka zinazooza na zile za plastiki ili kuipunguzia mzigo Halmashauri inayotumia asilimia kubwa ya fedha zake katika usafirishaji wa taka,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles