24.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 10, 2024

Contact us: [email protected]

JENNIFER LOPEZ AISAIDIA PUERTO RICO

NEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Jennifer Lopez, ameweka wazi kuguswa na tukio la kisiwa cha Puerto Rico kukumbwa na kimbunga na kusababisha uharibifu wa miundombinu na makazi.

Kutokana na tukio hilo, Jennifer amedai kuwa yupo tayari kutoa kiasi cha dola milioni moja, ambazo ni zaidi ya Sh bilioni mbili za Tanzania kwa ajili ya kusaidia kujengwa kwa kisiwa hicho.

Fedha hizo zinatokana na baadhi ya shoo alizozifanya kipindi cha hivi karibuni huko mjini Las Vegas, nchini Marekani.

Kisiwa hicho kinakadiriwa kuwa na jumla ya wakazi milioni 3.5,hivyo inadaiwa kuwa wazazi wa Jennifer wametokea kwenye kisiwa hicho na ndio maana ameonesha kuguswa zaidi kwa kuwa ni sehemu ya nyumbani kwake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles