24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Jenista atoa maagizo matano akifungua Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama ameagiza mambo matano kwa wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu huku akiwapongeza kwa kusimamia vizuri Uratibu wa shughuli za Serikali.

Mambo hayo nikuwa wabunifu katika utendaji kazi wao, kuwajibika, menejimenti kutenda haki bila kubagua, kutekeleza malengo waliyojiwekea na kutoa motisha kwa wafanyakazi wanaofanya vizuri hata wale walio katika ngazi za chini.

Akizungumza leo Jumatatu, Machi 18,2024 wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri Jenista amewapongeza wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii na weledi.

“Watumishi mmefanya kazi iliyotukuka mmefanya kazi kubwa, Naibu Waziri Ummy Nderiananga asante sana, Katibu Mkuu Dk. Yonazi umefanya kazi nzuri nawashukuru kwa utendaji kazi wenu,” amesema Waziri Jenista.

Hata hiyo, ameitaja Menejimenti kutenda haki kila siku bila ya kubagua ikiwa ni pamoja na kutoa motisha.

“Tusiache kutoa motisha kwa wafanyakazi wanaofanya vizuri na wale wa chini kwa sababu hakuna ambaye hana umuhimu,” amesema Waziri Jenista.

Pia, amewataka kuwa wabunifu katika utendaji kazi wao, kuwajibika, pamoja na menejimenti kutetekeleza malengo waliyojiwekea.

“Tuwe na ubunifu katika malengo yetu tuliyojiwekea 2024-2025 tutafute na kujadili njia ya kutekeleza ili tuweze kufanikiwa,” amesema Waziri Jenista.

Waziri Jenista amesema kuwa, majadiliano, mapendekezo na maamuzi yatakayotolewa katika mkutano huo yataleta tija na yataimarisha utendaji wa Ofisi hiyo.

Amesema katika mwaka huo wa 2023/24, Ofisi ya Waziri Mkuu – Fungu 25 na Fungu 37 iliidhinishiwa jumla ya Sh bilioni 43.3 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.

Amesema hadi Februari, 2024 fedha zilizopokelewa kwa Fungu 25 ni Sh bilioni 18.4 sawa na asilimia 105.3 na Fungu 37 ni Sh bilioni 22.2 sawa naasilimia 86.0 ya Bajeti iliyoidhinishwa.

Hata hivyo, kutokana na matukio ya dharura katika maadhimisho na sherehe za kitaifa; mazishi ya viongozi wa kitaifa; madeni ya wazabuni na Urejeshaji hali kutokana na maafa yaliyotokea maeneombalimbali ya nchi hususan Wilaya ya Hanang, Ofisi ya WaziriMkuu ililazimika kuomba fedha za ziada nje ya bajeti ili kukidhimahitaji katika matukio hayo.

“Ni matumaini yangu kuwa, utekelezaji wa bajeti hii tunayoendelea nayo ni matunda ya ushauri wenu katika kikao kama hiki kilichofanyika mwaka jana kabla ya kupitishwa kwa bajeti hiyo Bungeni,” amesema Waziri Jenista.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ummy Nderiananga amewapongeza watumishi kwa moyo wao wa kujitoa katika utendaji kazi.

Naye, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk. Jim Yonazi amewapongeza wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwa kufanya kazi vizuri jambo ambalo limekuwa likitoa faraja kubwa.

Dk. Yonazi ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu amesema katika kikao hicho watajadiliana taarifa ya utekelezaji ya kikao kilichopita kilichofanyika Machi 14, 2023 pamoja na kupitia taarifa ya utekelezaji ya Mpango wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka 2024-2025.

Awali, Mwakilishi wa Chama Cha Wafanyakazi (TUGHE) Mkoa wa Dodoma, Maisha Mbila amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kushirikiana, kupendana na kufanya kazi huku wakijua hakuna haki bila wajibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles