30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

JENEZA LA MARIA, CONSOLATA LAWATOA JASHO MAFUNDI

RAYMOND MINJA na FRANCIS GODWIN- IRINGA


MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Mandela Furniture, Zahara Kihwelo, iliyotengeneza jeneza la kuwazika mapacha wawili walioungana, Maria na Consalata Mwakikuti (22), amesema tangu wameanza kufanya kazi ya utengenezaji wa majeneza kwa zaidi ya miaka 25, hawajawahi kutengenea jeneza la aina yake kama hilo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, alisema iliwawia vigumu namna ya kulitengengeneza jeneza hilo kwa kuwa ni la kipekee kwani muundo wake ni moja, lakini kwa juu yanaonekana majeneza ni mawili yaliyoungana.

“Unajua hata sisi jana tulivyoenda na mafundi kuchukukua vipimo, tuliporudi tuliumiza vichwa sana jinsi ya kuliunda kwa kuwa unajua wale ndugu zetu walivyoungana.

“Lakini tunamshukuru Mungu kazi yetu imekwenda vizuri na sasa tumefanikiwa kutengeneza jeneza la aina yake ambalo hata mimi sijawahi kuliona,” alisema Kihwelo.

Mmoja wa mafundi waliotengeza jeneza hilo, Vivin Msangi, alisema katika maisha yake hajawahi kutengeneza jeneza moja litakalozika watu wawili walioungana.

Alisema utofauti wa jeneza hilo watakalozikwa Maria na Consolata, ni kubwa, refu na lenye mfuniko unaoonyesha ni majeneza mawili ndani ya moja.

“Hili ni jeneza la ina yake na la maajabu, ila namshukuru Mungu tumefanikiwa kwa asilimia 100 kulikamilisha, na mimi nimeingia kwenye historia ya kutengeneza jeneza litakalozika watu wawili walioungana,” alisema Msangi.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles