Na Christopher Msekena, Mtanzania Digital
Kiongozi wa Cutsleeve Records, Jdart Muzik, amewaweka tayari mashabiki zake kupokea ngoma mpya inayoitwa My Year, itakayotoka Ijumaa hii kwenye masoko yote ya muziki.
Jdart a.k.a Honkakuteki Boss, ameendelea kuwa kiungo muhimu cha muziki wa Afrika Mashariki, bara Asia na Jamaica kwa kuwaunganisha wasanii wa maeneo hayo kupitia lebo yake ya Cutsleeve Records.
Akizungumza na www.mtanzania.co.tz Jdart alisema wimbo MY YEAR utatoka mapema Ijumaa katika mfumo wa audio na video na utasambazwa kwenye mitandao yote muhimu ya kuuza muziki hivyo mashabiki waikimbilie burudani hiyo.
“Cutsleeve Records huwa hatubahaishi katika kuwapa raha mashabiki zetu, nimefungua mwaka 2024 na ngoma hii MY YEAR ambayo itakwenda kutoa tafsiri ya kile nitakachokifanya mwaka huu chini ya prodyuza wangu OG na Simpac hivyo naomba sapoti Afrika,” amesema Jdart.