25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

JAY-Z: TRUMP NI ‘MDUDU’ HATARI

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS wa Marekani Donald Trump amemjibu Jay-Z, baada ya mwanamuziki huyo wa rap kumuita ‘mdudu’ hatari na kumkaripia kwa namna anavyowachukulia watu weusi.

Akimjibu Jay-Z kwa matamshi yake hayo, ambayo yalikuwa yakilaumu kauli za kejeli anazodaiwa kuzitoa dhidi ya mataifa ya Afrika na, kupitia mtandao wa Twitter, Trump aliandika;

“Naomba mwambieni Jay-Z kuwa ni kwa sababu ya sera zangu kiwango cha Wamarekani weusi wasio na ajira kimeripotiwa kuwa cha chini kabisa kuwahi kurekodiwa,” alisema.

Wamarekani wenye asili ya Afrika wasio na ajira ni asilimia 6.8, kiwango ambacho ni cha chini kuwahi zaidi kurekodiwa.

Lakini wakosoaji wanasema kuwa kiwango cha uchumi kilianza kuimarika wakati wa Rais Barack Obama na kwamba ukosefu wa ajira miongoni mwa watu weusi bado uko juu kulinganisha na wazungu.

Lakini pia akihojiwa katika kipindi cha televisheni ya CNN cha Van Jones Show, Jay-Z alisema kuangazia viwango vya ukosefu wa ajira ni kukosa uelewa wa mambo.

“Tatizo tunalolizungumzia hapa si suala la ukosefu wa fedha pekee. Fedha hazileti furaha. Hii ni kushindwa kuelewa ukweli wa mambo. Hapa tunazungumzia kuwachukulia watu kama binadamu, hilo ndio suala kuu la muhimu,” Jay-Z alisema.

Aidha amesema kuchaguliwa kwa Trump kulikuja kwa bahati tu kutokana na kushindwa kutatuliwa kikamilifu kwa masuala kadhaa huko nyuma.

“Umepuliza manukato katika pipa la taka ni kwamba unawafanya wadudu hatari kufika. Unapopuliza kitu basi unasababisha kuzaliwa kwa wadudu hatari kwa sababu haungazii tatizo halisi.

“Hautoi taka nje, unaendelea kupuliza dawa juu yake ili kulifanya debe la taka lionekane safi. Vitu hivyo vinapozaliana na kukua, unazalisha mdudu hatari. Na kwa sasa mdudu hatari tuliye naye ni Donald Trump.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles