24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 30, 2023

Contact us: [email protected]

Jamhuri yawasilisha pingamizi rufaa ya Mbowe, Matiko itupwe

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Upande wa Jamhuri katika kesi ya pingamizi la kupinga uamuzi wa kufutiwa dhamana kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na umewasilisha pingamizi wakitaka pingamizi hilo litupwe.

Rufaa hiyo imeanza kusikilizwa leo Alhamisi Novemba 29 asubuhi, katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam mbele ya Jaji Sam Rumanyika anayesikiliza shauri hilo ambapo upande wa Jamhuri umewasilisha pingamizi hilo wakidai vifungu vya kisheria vilivyotuika si sahihi.

Wakili wa Serikali Mkuu, Dk. Zainabu Mango akiwasilisha hoja za pingamizi alidai vifungu vya sheria walivyotumia kuwasilisha rufaa si sahihi hivyo aliomba rufaa itupwe na kuongeza kuwa walitakiwa kuwasilisha rufaa chini ya kifungu cha sheria namba 359 na 361 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai.

Pia wanadai mwenendo wa kesi uliifikishwa mahakamani haujakamilika na haujachapwa hivyo hausomeki vizuri kwani kuna maneno yamekatika na mwandiko wa hakimu hausomeki vizuri katika baadhi ya maeneo.

Upande wa Jamhuri unaendelea kuwasilisha hoja huku upande wa warufani ukiongozwa na Wakili Peter Kibatala wakisubiri kujibu.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Ijumaa wili iliyopita iliwafutia dhamana washtakiwa Mbowe na Matiko, kwa kukiuka masharti ya dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,282FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles