25.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 4, 2022

DC Bariadi atoa agizo la pili Bodi ya Pamba

Derrick Milton, Simiyu

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu Festo Kiswaga ametoa muda mwingine wa siku tatu kwa Bodi ya Pamba nchini kuhakikisha inakamilisha ugawaji wa mbegu za pamba zilizobaki tani 1,600 ili kukamilisha tani 4,000 ambazo ndiyo mahitaji halisi wilayani humo.

Mwanzoni mwa mwezi huu, mkuu huyo wa wilaya, alitoa siku saba kwa bodi hiyo kuhakikisha inaleta mbegu za kwa wakulima kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi ya wakulima kukosa mbegu hizo.

Hata hivyo baada ya agizo hilo la kwanza, bodi ilianza kulitekeleza ndani ya siku mbili ambapo kwa siku moja bodi iliingiza zaidi ya tani 300 na kuzisambaza kwa wakulima.

Kiswaga ametoa agizo hilo leo wakati akiongea na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani humo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani.

“Ikiwa bodi hiyo haitakamilisha uletaji wa mbegu hizo ndani ya muda huo, nitahakikisha wafanyakazi wa bodi hiyo wanaondolewa kwenye nafasi zao kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,649FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles