22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Jaji Warioba, kikosi chake kunguruma Musoma

wariobaNA MWANDISHI WETU, MARA
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba pamoja na wajumbe wake, wanatarajiwa kunguruma mjini Musoma mkoani Mara katika mdahalo wa Katiba utakaofanyika Januari 24.
Taarifa iliyopatikana jana jijini Dar es Salaam na kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Gallus Abedi, mdahalo huo unatarajiwa kufanyika mjini Musoma katika Ukumbi wa MCC, kuanzia saa 8 mchana ikiwa ni mwendelezo wa midahalo ya aina hiyo inayoandaliwa na taasisi hiyo.
Alisema katika mdahalo huo mbali na Jaji Warioba, wengine watakaoshiriki ni waliokuwa wajumbe wa tume hiyo ambao ni Joseph Butiku, Profesa Mwesiga Baregu, Profesa Paramagamba Kabudi, Humphrey Polepole na Ali Saleh kutoka Zanzibar.
Abedi, alieleza kupitia taarifa hiyo kuwa mdahalo huo unalenga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuzingatia mambo muhimu yaliyomo katika Katiba inayopendekezwa, ikiwamo kuwapa fursa wananchi kusikiliza na kuelewa mambo muhimu na ya msingi kabla ya kuanza kwa upigaji kura ya maoni.
“Taasisi ya Mwalimu Nyerere haikusudii kukosoa au kuanzisha malumbano na mtu wala taasisi yoyote, zaidi ya kutimiza lengo lake la kutoa elimu ya uraia na kupanua uelewa miongoni mwa wananchi juu ya Katiba inayopendekezwa.
“Kama ilivyo kawaida ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa midahalo iliyokwishafanyika Jiji la Dar es Salaam na Mwanza, mdahalo huu utafanyika kwa njia ya amani, utulivu na bila hofu yoyote, na utakuwa mdahalo wa wazi kwa kila mtu kuhudhuria,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles