26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Jaji Ramadhan: Kesi ya ‘Samaki wa Magufuli’ ilinigusa

jaji agustino RamadhaniNA ELIZABETH HOMBO

JAJI Mkuu mstaafu wa Tanzania, Agustino Ramadhan amesema wahudumu wa meli ya wavuvi waliojumuishwa katika kesi ya ‘Samaki wa Magufuli’ hawakutendewa haki.

Jaji Ramadhan alisema alipata kutoa ushauri kwa Serikali ili wahudumu wa meli hiyo,waachiwe kwa kuwa hawakuwa na hatia, lakini hakusikilizwa.

Itakumbukwa kati ya Januari 10, 2009 na Machi 8, 2009, washtakiwa hao ambao ni Nahodha wa Meli, Hsu Chin Tai na Wakala wa Meli ya Tawariq 1, Zhao Hanquing, walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uvuvi haramu katika Ukanda wa Uchumi wa Tanzania.

Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu yaliyofanyika ofisini kwake jijini Arusha mwishoni mwa wiki, Jaji Ramadhani alisema kesi hiyo hataisahau kwa kuwa ilimgusa, kutokana na  watu wasiokuwa na hatia kujumuishwa.

“Wakati nikiwa Jaji Mkuu kesi moja ambayo kwa kweli ilinigusa ni ile ya meli ya wavuvi iliyoshikwa…ilinigusa sana kwa sababu kulikuwa na watu wengi mle nilishauri baharia na nahodha, wakamatwe, wale wafanyakazi wengine waachiwe, kwa bahati mbaya sikusikilizwa na kuna raia mmoja wa Kenya mpaka alifariki dunia,”alisema.

Jaji Ramadhani ambaye  sasa ni Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu ambayo makao makuu yake yako Arusha, alisema wakati akiwa Jaji Mkuu kesi hiyo iliwahi kufikishwa mbele yao ambayo ilimgusa na kumkosesha raha .

Alisema baadaye ya kukaa miaka miwili, iligundulika watuhumiwa hao hawakuwa na hatia na baadaye wakaachiwa huru.

Jaji huyo ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa Kuu  la Anglikana Zanzibar, alisema kesi nyingine ambayo ilimgusa ni ya babu Seya, lakini kwa kuwa bado iko mahakamani alikataa kuizungumzia.

“Kesi nyingine iliyonigusa ni ile ya Babu Seya, kwa sababu iko kwenye mahakama yetu hapa, naomba nisiizungumzie.

“Kwa kweli ilinigusa pia unakaa unajiuliza baba na watoto wake wa kiume wafanye haya waliyoyafanya? inakuwa ngumu kuingia akilini lakini sitaki kusema zaidi ya hapo. Tusubiri Mahakama ya Afrika itakavyoamua,”alisema Jaji Ramadhan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles