27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Jaguar avitaja vyanzo vya kipato chake

jaguarNAIROBI, KENYA

MKALI wa muziki nchini Kenya, Charles Njagua ‘Jaguar’, ameweka wazi vyanzo vyake vya fedha ambavyo vinampa jeuri ya kuongea kila kona nchini humo.

Msanii huyo ambaye ni mwanachama wa kupinga utumiaji wa dawa za kulevya wa (NACADA), amesema wasanii
wengi hawaumizi vichwa kutafuta njia ya kupata fedha nje ya muziki.

“Kila siku ninaumiza kichwa kuona jinsi gani nitaweza kuongeza kipato changu, kwa sasa kuna vitu ambavyo vinanipa fedha kama vile gereji, biashara ya kuuza magari na mambo mengine mbalimbali lakini bado havinitoshi.

“Wasanii wengi wanaangalia jinsi ya kupata fedha na kufanya matanuzi makubwa hasa kuvaa na kutoka na wanawake mbalimbali wakati huo hata nyumba au kiwanja hawana,” alisema Jaguar

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles