Mulongo kuwa mgeni rasmi Miss Albino

0
823

magesa-mulongoNA GEORGE KAYALA

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika shindano la Miss Albino Kanda ya Ziwa ambalo litafanyika Januari 29, mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, mratibu wa shindano hilo, Alexander Matowo, alisema Mulongo amekubali kushirikiana nao hatua kwa hatua ili kuhakikisha shughuli hiyo inafanikiwa kufanyika kwa utulivu na amani na kuwataka walemavu wote wa ngozi kujitokeza kushiriki.

“Mulongo amekubali kuwa mgeni rasmi katika shindano la kumsaka mlimbwende Albino, Kanda ya Ziwa na ameonyesha ushirikiano wa hali ya juu na kuwahamasisha viongozi wote wa kanda hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye shindano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika huko.

“Hata hivyo, amewataka watu wenye ulemavu wa ngozi kuanzia miaka 18 mpaka 30 kujitokeza kwa wingi kusaka nafasi hiyo,”
alisema Matowo. Shindano hilo linaendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la Save Vulnerable Foundation lenye makao yake Sinza jijini Dar es Salaam na tayari washindi wawili kutoka kanda ya Mashariki na Kaskazini wameshapatikana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here