25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

IVANKA KUWA MSAIDIZI WA BABA YAKE IKULU

WASHINGTON, MAREKANI


MWANAMITINDO, Ivanka Trump, amejiunga rasmi na Serikali ya baba yake ambapo atahudumu kama mfanyakazi asiyelipwa, kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani, White House jana.

Hatua hiyo inakuja baada ya wataalamu wa maadili kuhoji na kukosoa mpango wa awali wa binti huyo wa Rais Donald Trump wa kutaka kuhudumu katika wadhifa usio rasmi.

Ivanka (35), ambaye cheo chake rasmi kinakuwa msaidizi wa rais, amesema amesikia ‘maswali ambayo baadhi ya watu walikuwa wakihoji kuhusu hatua yake ya kumshauri rais katika nafasi yake kama mtu binafsi.

Mumewe, Jared Kushner, tayari ni mshauri mwandamizi wa Rais Trump.

Kupitia taarifa yake White House imesema ina furaha kuwa Ivanka Trump amechukua hatua hii isiyotarajiwa katika nafasi yake kama binti wa rais.

Trump alisema kupitia taarifa yake  amekuwa akifanya kazi kwa nia njema na kundi la washauri wa Rais Ikulu pamoja na mshauri wake binafsi kujadili kuhusu jukumu lake.

Wataalamu kuhusu maadili walilalamika ilipobainika wiki iliyopita kuwa Trump angepewa ofisi White House pamoja na kibali cha usalama cha kuingia na kutoka Ikulu hiyo ilihali si sehemu ya wahudumu wa rais.

Wakosoaji walisema kazi ya  Trump inapaswa kufanywa rasmi ndipo aweze kudhibitiwa na sheria kuhusu uwazi wa maafisa wa serikali pamoja na maadili.

Aidha, adhibitiwe na sheria kuhusu mgongano wa maslahi.

Wakili wa Trump, Jamie Gorelick, alisema mteja wake atawasilisha nyaraka stahili za kufichua utajiri wake kwa mujibu wa sheria kuhusu maadili ya watumishi wa umma Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles