29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

MGOMBEA AAHIDI KUBORESHA BIASHARA YA UKAHABA KENYA

KISUMU, KENYA


MGOMBEA wa ugavana katika Kaunti ya Kisumu ameibua mjadala mkali baada ya kuwaahidi makahaba kuwatafutia wateja na mazingira bora ya biashara yao, iwapo atachaguliwa katika Uchaguzi Mkuu Agosti 8, mwaka huu.

Dk. Hezron McObewa, ambaye amedhamiria kumng’oa Gavana wa sasa Jack Ranguma, alisema atakuwa akiandaa mikutano ya kimataifa mjini humo itakayovutia wageni wengi, ambao watakuwa wakiwalipa makahaba ‘bei za kimataifa’.

Mwanasiasa huyo alikuwa akizungumza alipokutana na mahakaba 300 katika taasisi ya Goan mjini hapa.

“Watu hawa hulipa vizuri wanapozuru nchi za kigeni na wenzenu wanaohudumu katika nchi zao hupata hadi Sh 200,000 za Kenya (Sh milioni 4 za Tanzania) kwa usiku mmoja.”

“Ni mikutano mikubwa ambayo huwaleta wateja ambao watawalipa donge nono,” alidai.

Aliongeza: “Watakapokuja, watawalipa bei za kimataifa kama walivyozoea wanapoenda katika nchi nyingine. mtashangaa na kufurahi!” alisema.

Dk. McObewa ni miongoni mwa wanasiasa ambao wanatumia kila mbinu kuvutia wapiga kura kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.

“Biashara yenu itakuwa ya maana kama kuna wanaume wenye mabunda ya noti mfukoni, hiyo ni fursa nzuri ya kuboresha, kutengeneza ajira na kuongeza kipato,” alisema.

Mgombea huyo alimshutumu Ranguma kwa kutojali mahitaji ya makahaba hao ambao ni wanachama wa chama cha ushirika (Sacco) cha makahaba wa Kisumu.

Aliwataka wasimchague Ranguma kama wanataka kufanikiwa kutokana na huduma na wateja atakaoleta kuwasaidia.

Wengine walio kwenye kinyang’anyiro cha ugavana wa kaunti hiyo ni Seneta wa Kisumu Prof. Anyang’ Nyong’o, Naibu Gavana wa Kisumu, Ruth Odinga, Msanifu Ujenzi Chris Ondiek, Mwenyekiti wa Chama cha Jubilee katika kaunti hiyo, Atieno Otieno.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles